Saturday, March 31, 2012

Marekani yaanzisha utekelezaji wa vikwazo kwa wanunuzi wa mafuta Iran

Raisi wa Marekani Barack Obama
Raisi wa Marekani Barack Obama
REUTERS/Larry Downing
 
Fukuto la mgogoro wa Iran limeendelea ambapo raisi wa marekani Barack Obama amethibitisha kuanzishwa kwa vikwazo mahususi kwa washirika na wanunuzi wa mafuta yanayopatikana nchini Iran.

Katika taarifa yake raisi Obama alisema washirika wa marekani wakigomea mafuta ya Iran hawatadhurika kwakuwa kuna mafuta ya kutosha katika soko la dunia.
Mpango huo utaiwezesha Marekani kuchukua hatua dhidi ya benki za kigeni ambazo bado zinajihusisha na mfauta ya Iran.

Iran inakabiliwa na shinikizo la kimataifa juu ya wasiwasi wa nchi hiyo kujitajirisha kupitia mpango wake wa uzalishaji wa nyuklia jambo ambalo mataifa ya magharibi yanaituhumu Iran kuzalisha silaha za nyuklia.










 

Jeshi lililofanya mapinduzi Mali latafuta msaada kupambana na mashambulizi ya Tuareg.

Nchi ya Mali kama inavyoonekana katika ramani.
Nchi ya Mali kama inavyoonekana katika ramani.
RFI/Anthony Terrade
 
 
Kiongozi wa jeshi lililofanya mapinduzi ya serikali nchini Mali Captain Amadou Sanogo ameomba msaada kutoka kwa nchi nyingine kuendeleza mapambano na kundi la waasi wa Tuareg kutokana na askari wake kuzidiwa hususan katika mji mkuu wa kaskazini.

Jeshi la Mali limearifu mapema jumamosi kuwa limeyarudisha majeshi yake nje ya mji miwili iliyopo kaskazini mashariki mwa nchi hiyo masaa machache baada ya kundi la waasi wa tuareg kuwashambulia na kuwatoa nje ya mkakati wao mjini kidal.

Gao ni mji mkubwa kaskazini mwa mali ambako kumesalia mikononi mwa utawala mpya wa Junta ambao umeendelea kusisitiza kuwa majeshi yameondolewa Ansogo na Bourem ili kutekeleza maazimio yao huko Gao.

Umoja wa nchi za kanda ya Magharibi mwa Afrika, ECOWAS, umelaani kitendo cha wanajeshi kuupindua utawala , huku nchi hizo zikitishia kuiwekea vikwazo na kuwapa saa 72 kuondoka madarakani au kuwaadhibu kwa kuweka vikwazo vya kiuchumi.


 


Kundi la nchi zinazoinukia kiuchumi duniani, BRICS, linakutana nchini India na kuweka azimio la kuzishinikiza nchi za maghiribi kuruhusu usawa kwenye taasisi za kuchumi duniani likiwemo Shirika la Fedha Duniani, IMF.

Katika azimio lao la kwanza la mkutano huo unaofanyika New Delhi nchini India, mataifa hayo ambayo ni Brazil, China, Afrika Kusini, Urusi na India yamepaza sauti zao kuhusu kasi ndogo ya mabadiliko ndani ya Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, na pia kutaka kuwepo kwa uwazi katika mchakato wa kumpata rais ajaye wa taasisi hiyo.

Wakiwa na matumaini ya kuleta mabadiliko ambayo yatawapa nguvu ya haki ya kupiga kura katika maamuzi mbalimbali ndani ya IMF, bado matumaini hayo yako mashakani kwani yanategemea pia uungwaji mkono wa Marekani.

Mashaka hayo yanazidi kuwa makubwa hasa linapokuja suala la mtafaruku wa kundi la G7 pamoja na kukosa nafasi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambapo Brazil na India zimekuwa zikipigania kupata uwakilishi wa kudumu kwa muda mrefu sasa.

Wito wa kusitisha kuyumba kwa uchumi duniani

Tamko la azimio hilo limetoa wito kwa nchi zilizoendelea kuacha kutengeneza mianya ya kuyumba kwa uchumi wa dunia. Kauli hiyo imekuwa ikitolewa mara kwa mara na mataifa yanaoendelea ambayo uchumi wake umeathirika na mtikisiko wa kuiuchumi ulioikumba dunia katika miaka ya hivi karibuni.
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, nchi nchi pekee ya kiafrika katika kundi la BRICS Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, nchi nchi pekee ya kiafrika katika kundi la BRICS
Hata hivyo kundi hilo la BRICS hadi sasa bado halijaonyesha juhudi za wazi za kuunga mkono mgombea yoyote kati ya watatu wanaotarajiwa kuchukua nafasi ya urais wa Benki ya Dunia kutoka kwa Mmarekani Robert Zoellick.

Waziri wa Viwanda na Biashara wa India Fernando Pimentel aliliambia Shirika la Habari la Reuters siku moja kabla ya kuanza kwa mkutano huo kuwa, nchi yake ina matumaini na ujumbe utakaotolewa katika mkutano huo utafanikiwa na kuleta mabadiliko ya sera ambazo kundi la BRICS linazitazama kama zisizo na usawa kutokana na maamuzi ya mataifa ya Ulaya na Marekani.
 
Muungano wa masoko ya kifedha

Mataifa hayo matano ambayo yanakusanya karibu ya nusu ya watu wote duniani yanatarajiwa kutangaza hatua za umoja wa kiuchumi miongoni mwao ikiwa ni pamoja na kuunganisha masoko yao ya fedha na mpango wa kuwa na mfuko wa fedha kwa ajili ya maendeleo pamoja ndani ya Benki ya Dunia

Kundi hilo limekuwa likikosolewa kwa muundo wake hauwezi kuwa na mafanikio, lakini mwanauchumi Jim O´Neill anasema kuwa kitendo cha nchi hizo kukutana tu, kinatosha kufikisha ujumbe kwa wahusika.
Mwanauchumi huyo analitazama kundi hilo kama kengele inayolikumbusha kindi lingine la G7 na mataifa ya magharibi kuwa yanahitaji kufanya mabadiliko na kutoa fursa kwa mataifa ya G20, IMF na Benki Ya Dunia kushiriki katika masuala ya fedha ya kidunia kwa uhuru zaidi.

Mkutano huo pia utajadili masuala mengine ya utawala,mabadiliko ya hali ya hewa duniani, ugaidi, pamoja na masuala ya chakula usalama.
Suala la hali ya usalama katika eneo la mashariki ya kati pia litajadiliwa katika mkutano huo pamoja na mpango wa nyuklia wa Iran.





No comments:

Post a Comment