Saturday, March 31, 2012

 


Nchi ya Mali kama inavyoonekana katika ramani.
RFI/Anthony Terrade
Kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi katika nchi ya Afrika Magharibi Mali Kapteni Amadou Sanogo ameomba msaada kutoka kwa mataifa ya kigeni baada ya waasi wa Tuareg kuuteka mji wa Kaskazini Mashariki Kidal.
Jeshi la Mali lilisema kuwa limewaondoa wanajeshi wake katika miji miwili ya Kaskazini mwa nchi hiyo, saa chache baada ya waasi wa Kituareg kuwatimua kutoka mji muhimu wa Kidal. Kwa mujibu wa taartifa iliyotolewa na jeshi, vikosi viliondoka katika miji ya Ansogo na Bourem ili kuimarisha nafasi zao katika mji wa Gao. Gao ni mji mkubwa Kaskazini mwa Mali ambao ungali mikononi mwa jeshi la Mali linaloongoza nchi kwa sasa.
Hali sasa ni mbaya
Ombi la Sanogo lilitolewa jana wakati ambapo uongozi wa jeshi hilo uliodumu wiki moja, na ambao tayari umetengwa na washirika wake wa nje unakabiliwa na uwezekano wa kuwekewa vikwazo vya kiuchumi kutoka kwa nchi jirani vinavyoweza kuikwamisha nchi hiyo. Nchi hizo zinataka kurejeshwa kwa utawala wa kikatiba nchini humo.

Jumuiya ya ECOWAS imetishia kuiwekea vikwazo Mali ikiwa haitarejesha utawala wa kikatiba Jumuiya ya ECOWAS imetishia kuiwekea vikwazo Mali ikiwa haitarejesha utawala wa kikatiba
Kiongozi wa mapinduzi Kapteni Sanogo aliwaambia waandishi habari katika ikulu ya rais ambayo sasa ndiyo makao makuu ya kijeshi kuwa waasi wanaendelea kuishambulia nchi yao na kuwasumbua raia. Aliongeza hali sasa ni mbaya, jeshi linahitaji msaada kutoka kwa marafiki wa Mali ili kuwaokoa wananchi na kuilinda himaya ya nchi hiyo. Baada ya mapigano makali, waasi wa Kituareg pamoja na kundi moja la Kiislamu lililojihami ambalo linawaunga mkono waasi hao, waliingia mji wa Kidal, ambao ni kilomita 1,000 kutoka mji mkuu Bamako.
Mapigano kuendelea
Katika tuvuti yake, kundi la Azawad National Liberation Movement MNLA lilisema litaendelea na mashambulizi dhidi ya miji mingine miwili mikuu katika eneo hilo ili kuwaondoa wanajeshi wa Mali. Wapiganaji wa kundi la MNLA wanashirikiana na wanamgambo wa Kiislamu wa Ansar Dine yaani “Walinzi wa Imani” katika lugha ya Kiarabu.
Mashambulizi ya Tuareg yamesababisha takribani watu 200,000 kukimbia makwao katika eneo la kaskazini mashariki mwa Mali ambalo pia ni maarufu kwa ulanguzi wa silaha na dawa za kulevya. Kutwaliwa kwa mji wa Kidal, ambao ndio mji mkuu wa jimbo la Kaskazini Mashariki unaopakana na Niger na Algeria ni mafanikio makubwa kwa waasi hao ambao tayari wametwaa udhibiti wa miji mingine mikuu ya Tessalit na Aguelhok katika mkoa huo.

Nchi za Umoja wa sarafu ya Euro zimepiga hatua zaidi mbele katika juhudi za kukabiliana na mgogoro wa madeni baada ya kufikia makubaliano ya kuongeza fedha katika mfuko wa uokozi.

Mawaziri wa fedha wa nchi zinazotumia sarafu ya Euro wamekubaliana kuongeza uwezo wa kifedha hadi Euro Bilioni 700 ili kuepusha migogoro mingine ya madeni kutokea katika nchi zao. Masoko na washirika wa nchi za G 20 wamezipokea habari hizo kwa faraja.

Mawaziri hao wa nchi 17 za Umoja wa sarafu ya Euro wameamua kuiunganisha mifuko miwili ya uokozi na hivyo kupata Euro Bilioni 500 zitakazowekwa tayari kuikabili dharura yoyote itakayotokea baina ya sasa na kati kati ya mwaka ujao. Fedha hizo ni nyongeza ya Euro Bilioni 200 ambazo zimekwishawekwa tayari kwa ajili ya kuziokoa Ugiriki, Ireland na Ureno.

Mkurugenzi wa IMF Christine Lagarde na Waziri wa fedha wa Ujerumani Wolfgang Schäuble Mkurugenzi wa IMF Christine Lagarde na Waziri wa fedha wa Ujerumani Wolfgang Schäuble


Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF Christine Lagarde ameafikiana na uamuzi huo na amesema kuwa utalisaidia shirika lake, linalotoa mikopo duniani, kuweza kuongeza fedha ili kuzuia kuenea kwa athari zinazotokana na mgogoro wa madeni barani Ulaya, ikiwa litahitajika kufanya hivyo

Kutokana na shinikizo la kimataifa kuwataka waukabili mgogoro wa madeni ambao umeshachukua muda wa miaka miwili na kutokana na matatizo ya bajeti ya Uhispania ,mawaziri hao wamefikia makubaliano yenye lengo la kuyapa imani masoko ya fedha.

Marekani imesema makubaliano ya mawaziri wa nchi za Umoja wa Sarafu ya Euro yameimarisha imani katika eneo la Euro.Msemaji wa wizara ya fedha ya Marekani ameeleza kuwa, katika miezi kadhaa iliyopita viongozi wa Ulaya wamepiga hatua madhubuti katika kuukabili mgogoro wa madeni.

 

Marekani yaanzisha utekelezaji wa vikwazo kwa wanunuzi wa mafuta Iran

Raisi wa Marekani Barack Obama
Raisi wa Marekani Barack Obama
 
Fukuto la mgogoro wa Iran limeendelea ambapo raisi wa marekani Barack Obama amethibitisha kuanzishwa kwa vikwazo mahususi kwa washirika na wanunuzi wa mafuta yanayopatikana nchini Iran.

Katika taarifa yake raisi Obama alisema washirika wa marekani wakigomea mafuta ya Iran hawatadhurika kwakuwa kuna mafuta ya kutosha katika soko la dunia.
Mpango huo utaiwezesha Marekani kuchukua hatua dhidi ya benki za kigeni ambazo bado zinajihusisha na mfauta ya Iran.
Iran inakabiliwa na shinikizo la kimataifa juu ya wasiwasi wa nchi hiyo kujitajirisha kupitia mpango wake wa uzalishaji wa nyuklia jambo ambalo mataifa ya magharibi yanaituhumu Iran kuzalisha silaha za nyuklia.

No comments:

Post a Comment