Syria yakubali muda wa kusimamisha ghasia
Syria imekubali tarehe 10 Aprili kama muda wa mwisho kuanza
kutekeleza mpango wa amani uliopendekezwa na mjumbe wa pamoja wa Umoja
wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Kofi Annan.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Susan Rice ameliambia Baraza la Usalama kuwa Annan amesema kwamba Syria imekubali kuwa ifikapo tarehe 10 April itakuwa imeondoa wanajeshi wake na zana nzito nzito za kijeshi kutoka miji yenye harakati za upinzani.
Ujumbe wa kulinda amani
''Bwana Kofi Annan amekuwa akiwasiliana na maafisa wa serikali yetu mara kwa mara, na pande zote zimepata muafaka wa kufanya kazi pamoja, kutafuta njia nzuri za kusimamia utekelezwaji wa mpango wa amani wenye vipengele sita kwa kuheshimu uhuru wa Syria''.
Lakini ridhaa ya Syria imepokelewa kwa mashaka na baadhi ya nchi, kama alivyoeleza Susan Rice, balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa.
Mashaka juu ya ''nia njema''
Na wana mashaka juu ya wema wa nia ya Syria juu ya mpango huo. Lakini kwa ujumla wanachama wa baraza la usalama wameelezea utashi wao kutafakari pendekezo la bwana Annan kuweka ujumbe wa kulinda amani, iwapo kweli ghasia zitasimamishwa.''
Urusi ambayo siku zilizopita ilitaka serikali ya Syria na waasi wasimamishe matumizi ya nguvu kwa wakati mmoja, sasa inakubaliana na mpango wa Kofi Annan unaoitaka serikali kuchukua hatua ya kwanza.
Wanadiplomasia wamesema kwamba mpango wa amani wa Kofi Annan wenye vipengele sita, unataka usitishwaji kamili wa ghasia zote katika masaa 48 baada ya tarehe 10 April.
Mbali na na kusimamishwa kwa vurugu, mpango wa Annan unahimiza mazungumzo ya kisiasa yatakayoongozwa na wasyria wenyewe, haki ya watu kuandamana, na kufunguliwa kwa watu waliwekwa kizuizini kimabavu.
30 zaida wafa katika ghasia
Ripoti hizo zilisema vikosi vya serikali vimeingia kwa vifaru katika miji yenye uasi, na kuwakamata wanaharakati na pia kuchoma na kubomoa nyumba zao.
Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Syria lenye makao yake mjini London, jana limesema kuwa watu 10,108 wamekwishauawa katika mgogoro wa Syria.
No comments:
Post a Comment