Thursday, September 6, 2012


Rais Barack Obama na rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton
Chama cha Democrats nchini Marekani kimemteua rasmi Barack Obama, rais wa sasa wa nchi hiyo, kugombea nafasi ya urais kwa kipindi kingine cha miaka minne.

 Obama anatarajiwa kukubali uteuzi huo leo usiku ambapo pia atatoa hotuba ambayo inatazamiwa kuzungumzia mpango wa "kwenda mbele", ambayo ndio kaulimbiu ya kampeni yake ya uchaguzi


Maoni ya hivi karibuni yanaonyesha kuwa sera ya huduma za afya na uhamiaji zinampelekea rais Obama kumzidi mpinzani wake katika uchaguzi huo Mitt Romney wa chama cha Republican, hususan kwa wanawake na wapiga kura wa kilatino katika majimbo yanayoweza kubadilika katika upigaji kura, likiwemo jimbo la North Carolina.

No comments:

Post a Comment